Michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya hatua ya Makundi imeendelea tena usiku wa November 4 kwa michezo nane kupigwa ikihusisha timu kutoka Kundi E, F, G na H, zikiwa timu zote zilizocheza usiku wa November 4 zilikuwa zinacheza mchezo wake wa nne, klabu ya FC Bayern Munich iliikaribisha Arsenal katika dimba la Allianz Arena.
FC Bayern Munich wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa Arsenal mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa nyumbani wa Arsenal Emirates, wamelipiza kisasi kwa kuifunga Arsenal jumla ya goli 5-1 na kutimiza jumla ya point 9 katika msimamo wa Kundi F huku ikiongoza kwa utofauti wa magoli 10 ya kufunga na kufungwa.
Magoli ya FC Bayern Munich yalifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 10, Thomas Muller aliyefunga goli mbili dakika ya 29 na 89, David Alaba dakika ya 44 na Arjen Robben dakika ya 55 na Arsenal kuambulia goli moja lililofungwa na Oliver Giroud dakika ya 69, kwa matokeo hayo klabu ya Arsenal itakuwa na nafasi ndogo ya kufuzu kwenda hatua ya 16, kwani inatakiwa ishinde kwa idadi kubwa ya magoli katika mechi zake mbili zilizosalia huku ikiomba dua Olympiakos ipoteze kwa kufungwa mechi zote mbili zilizosalia.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa November 4
Kundi E
-
Barcelona 3 – 0 BATE Borisov
-
Roma 3 – 2 Bayer Leverkusen
Kundi F
-
Bayern Munich 5 – 1 Arsenal
-
Olympiakos 2 – 1 Dinamo Zagreb
Kundi G
-
Chelsea 2 – 1 Dynamo Kyiv
-
Maccabi Tel Aviv 1 – 3 FC Porto
Kundi H
-
Gent 1 – 0 Valencia
-
Lyon 0 – 2 Zenit St. Petersburg
Video ya magoli ya FC Bayern Munich Vs Arsenal
https://youtu.be/Og9m9Nr0iSQ
Video ya magoli ya FC Barcelona Vs BATE Borisov
https://youtu.be/5P7AbZ2ZL2E
Video ya magoli ya Chelsea Vs Dynamo Kyiv
https://youtu.be/WLJkCHkqWuA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.