Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea leo October 20 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya. Miongoni mwa mchezo uliyovuta hisia za mashabiki wengi wa soka ni mchezo kati ya Arsenal dhidi ya FC Bayern Munich ya Ujerumani ambayo kabla ya mchezo huo kumalizika ilikuwa haijapoteza mechi hata moja.
Kikubwa kilichokuwa ni kivutio cha mechi hiyo ni mashabiki wa soka walitaka kuona kama Arsenal ingevunja rekodi yake yenyewe, Arsenal ambayo ilikuwa imeshapoteza michezo miwili ya awali, ilikuwa haijawahi kupoteza mechi tatu mfululizo za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Klabu ya Arsenal ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani imeibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya FC Bayern Munich.
Mchezo ambao ulikuwa hukichezwa kwa tahadhari kwa timu zote hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika kulikuwa hakuna timu iliyokuwa imeona nyavu za mwenzake. Arsenal ambayo ilikuwa na wakati mgumu wa kutaka kufufua matumaini ya kutaka kufuzu hatua ya 16 ilianza kupachika goli dakika ya 77 kupitia kwa Olivier Giroud kabla ya dakika ya 90 Mesut Ozil kuhitimisha kwa kufunga goli la pili.
Video ya Magoli ya Arsenal Vs FC Bayern Munich
https://youtu.be/SHPhtuP3cTg
Video ya magoli ya BATE Borisov Vs Barcelona
https://youtu.be/yt4a-CF-YIQ
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.