Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo amesema Daraja la Gichameda kata ya Magugu limekamilika na kuanza kutumika likiunganisha Gichameda na vijiji vingine vya kata ya hiyo ya Magugu ambapo mpaka kukamilika kwake ni zaidi ya shilingi Bilioni1 zimetumika..
Sillo amesema kukamilika kwa daraja hilo kunatoa fursa kwa Wananchi kuweza kusafirisha mazao yao kwa urahisi huku akiwataka Wananchi kuonesha uchungu kwenye kodi zao kwa kulitunza daraja hilo ili lidumu kwa muda mrefu huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zimewezesha ujenzi wa daraja hilo.
Akielezea mchanganuo wa fedha hizo Meneja wa TARURA wilaya ya Babati Mhandisi Nombo, amesema Gravel yenye ukubwa wa km 9.3 shilingi milioni 168,021,500, kuchonga km 9.3 shilingi milioni 20,460,000, kunyanya tuta km 1.8 shilingi milioni 221,000,000, Pipe Culvert 19 kwa shilingi 114,000,000, River training km 2 sawa na shilingi 167,750,000, ukuta wa mawe kuzuia maji shilingi 97,500,000, daraja mita 22 shilingi 360,283,500 pamoja na gharama za awali shilingi milioni 43,400,000 ambazo jumla yake ni shilingi Bilioni 1,191,915,000.