Ufalme wa Eswatini umekanusha ripoti kwamba ulikuwa ukitoa utaifa kwa raia kutoka kusini mwa Afrika ili kujaza uhaba wa wanaume nchini humo.
Inafuatia barua bandia inayodaiwa kuandikwa na Mfalme Mswati wa Tatu akielezea wasiwasi wake kuhusu “uhaba wa wanaume” katika ufalme huo.
Barua hiyo ilidai mfalme angewezesha wanaume walio tayari kutoka kusini mwa Afrika kuoa wake na kupata nyumba za bure kutoka kwa ufalme. huo
“Umma unaarifiwa kuwa ilani hii inayosambaa ni bandia,” serikali ya Eswatini ilisema katika taarifa fupi iliyotumwa kwenye X.
Haijabainika ni nani aliyeandika barua hiyo ambayo iliwasisimua baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutoka kusini mwa Afrika.