Nchi ya Ufaransa imetangaza kuwa inasitisha rasmi misaada ya maendeleo na bajeti kwa nchi ya Burkina Faso, tangazo linaloteolewa siku chache kupita tangu nchi hiyo na Mali zitangaze kuunga mkono mapinduzi ya Niger, imesema taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Paris.
Tangazo hilo linakuja baada ya serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso kusema kwamba ingechukulia uingiliaji wowote wa silaha dhidi ya viongozi wa mapinduzi katika nchi jirani ya Niger kama tangazo la vita.
Serikali ya kijeshi nchini Mali imechukua msimamo huo huo.
Hatua hii inakuja wakati makataa ya jumuiya ya Afrika Magharibi Ecowas kwa viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Niger kurejesha utulivu wa kikatiba na kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa Mohamed Bazoum ilipotimia Jumapili jioni.
Ecowas bado haijatoa tamko kuhusu hatua inayofuata ambayo ni pamoja na kuingilia kijeshi.
Tume hiyo hapo awali ilisema kuwa hilo la hatua za kijeshi lingekuwa “chaguo la mwisho” iwapo mbinu zingine zote za kisiasa na kidiplomasia zitashindwa.
Tazama pia…