Ikiwa na maeneo 2,600 tu ya ibada kwa Waislamu milioni tano, Ufaransa ina uhaba wa misikiti – na kupata vibali na ufadhili wa maeneo mapya ya kidini ni ngumu sana.
Hilo linawaacha waumini wengi wakihangaika kutafuta mahali pa kuswalia hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Kwa urahisi kabisa, tunahitaji nafasi,” anasema Abdellah, mmoja wa makumi ya watu wanaopanga mstari kuingia kwenye msikiti wa Javel kusini-magharibi mwa Paris kwa ajili ya sala ya Ijumaa.
“Tunasali kwa zamu mbili, tumejaa ndani, sio vizuri. Ni ngumu sana, na wakati wa Ramadhani ni mbaya zaidi. Tunaomba upesi iwezekanavyo ili tusichoke.”
Msikiti huo, ulio kwenye ghorofa moja ya jengo la ofisi ya matofali, ulifunguliwa mwaka wa 2003 na nafasi kwa karibu waabudu 350. Lakini kwa miaka kadhaa sasa, imejikuta ikihangaika kuwapa nafasi wale wanaokuja kusali.
“Kwa bahati mbaya sehemu ya kusini ya Paris haitumiki vizuri kwa maeneo ya ibada ya Waislamu. Huu ndio msikiti wa pekee kusini-magharibi mwa Paris,” anasema mkuu wa idara, Najat Benali.