Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu OCHA, zaidi ya malori 30 ya misaada yalifika Gaza siku ya Jumapili, na kuashiria msafara mkubwa zaidi katika eneo lililokumbwa na vita la Palestina tangu kuanza tena kwa usafirishaji zaidi ya wiki moja iliyopita.
Msafara huo, unaojumuisha malori 33 yaliyokuwa yamebeba vifaa muhimu kama vile maji, chakula, na mahitaji ya matibabu, uliingia Gaza kupitia kivuko cha mpaka cha Rafah na Misri.
“Huu ni uwasilishaji mkubwa zaidi wa misaada ya kibinadamu tangu tarehe 21 Oktoba, wakati utoaji mdogo ulianza tena,” ilisema.
Tangu kuanza kwa usafirishaji, malori 117 yameingia Gaza kupitia kivuko. Eneo hilo lenye watu milioni 2.4, linakabiliwa na vizuizi vikali na mashambulizi ya anga ya Israel.