Kila siku asubuhi huwa nazisogeza Headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account zangu za Twitter, Facebook na Instagram kupitia jina la @millardayo.
Magazeti yote ya Tanzania leo Nov 29 2016 na habari zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho pic.twitter.com/n6Uyi3PzrF
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
Moja kati ya stori kubwa kwenye magazeti ya leo ni kuhusu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili MNH kutangaza kuanza kwa huduma ya uchunguzi na matibabu ya Homa ya Ini (Hepatitis B) ambayo imetajwa kuwa hatari zaidi ya UKIMWI kutokana na kuenea kusababisha maambukizi na vifo kwa idadi kubwa.
Kwa mujibu wa Dr. John Lwegasha ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Tumbo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema kuwa utafiti umeonesha kuwa Tanzania kwenye kila watu 100 basi kuna watu 8 walioambukizwa ugonjwa huu.
#MAJIRA Hospitali ya Taifa Muhimbili inatarajia kuanza uchunguzi wa virusi vya homa ya Ini Hepatitis B, Dec 1 na kutoa tiba bure ya ugonjwa pic.twitter.com/6yUInVD0vx
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
BAADA ya gharama za matibabu ya ugonjwa wa homa ya ini (Hepatitis B) kuwa janga linalofanya Watanzania wengi kupoteza maisha yao kutokana na kushindwa gharama zake, serikali sasa imepata ufadhili wa tiba ya ugonjwa huo kwa kipindi cha miaka mitano.
Tiba hiyo itaanza kutolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam ambako inatarajia kuanza kufanya uchunguzi wa virusi hivyo na kutoa tiba ya bure kwa kutumia dawa ya Tenofovir kuanzia Desemba Mosi, mwaka huu.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, daktari bingwa wa magonjwa ya ini na matumbo, John Rwegasha alisema utaratibu wa kutoa huduma hiyo utafanyika kwa ushirikiano na ufadhili wa wadau wa maendeleo kutoka Kitengo cha Udhibiti wa Magonjwa nchini Marekani.
“Tiba hii hasa ni katika kupima wingi na kinga ya virusi hivi mwilini pamoja na tiba za ugonjwa huu kwa kutumia dawa hiyo kwa kipindi chote cha miaka mitano ya mpango huo,” “Mpango huu una lengo pia la kujenga uwezo wa ndani wa nchi ili kufanya tiba kuwa endelevu katika miongozo inayotolewa juu ya tiba ya ugonjwa huu na Shirika la Afya Duniani (WHO) hususan katika nchi zinazoendelea kama Tanzania.” – Dk Rwegasha
Alisema asilimia tano ya wagonjwa wa homa ya ini hawaponi, hivyo kuendelea kuleta maambukizi sugu mwilini na hasa kwenye ini na figo na hivyo baada ya miaka 10 na kuendelea, ini husinyaa na kupata magonjwa nyemelezi, tumbo kujaa maji na figo kushindwa kufanya kazi huku asilimia 95 ya wagonjwa miili yao hujitengenezea kinga za kupambana na virusi ndani ya miezi sita na kupona kabisa.
“Mgonjwa mwenye ugonjwa huu inabidi kutumia dawa hizo kwa muda mrefu usiopungua miaka mitano kumwezesha mgonjwa kujitengenezea kinga inayojiwezesha kupambana na ugonjwa huo,” alieleza Dk Rwegasha.
Alisema ugonjwa huo unashabihiana na ugonjwa wa Ukimwi hasa katika njia za maambukizi kama kufanya ngono zisizo salama, kuchangia sindano na vitu vyenye ncha kali, kupewa damu yenye maambukizi na pia kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha, alisema inakadiriwa kuwa watu wanane kati ya 100 wana maambukizi ya ugonjwa huo na kwamba asilimia 60 ya wagonjwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili waliokutwa na saratani ya ini, inatokana na maambukizi ya virusi hivyo.
“Utafiti unaonesha kuwa uwezekano wa kupata ugonjwa huu ni mara kumi zaidi ya maambukizi ya Ukimwi ingawa changamoto kubwa ni uelewa kwa jamii ukilinganisha na ugonjwa wa Ukimwi, kifua kikuu na magonjwa mengine ya kuambukiza,” alifafanua na kutoa mwito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili wafanyiwe uchunguzi zaidi na kupata tiba baada ya kupata ufadhili huo ambao ulikuwa ukimhitaji mgonjwa kutumia fedha nyingi.
Alisema hata hivyo utaratibu utabaki ule ule wa mgonjwa kufika hospitali kwa gharama za kufungua faili, kumuona daktari na kupima vipimo vya awali kisha kuingia katika huduma ya kupima wingi wa virusi na pia kinga ya mwili na kupatiwa dawa kama itahitajika.
Alisema kwa kawaida dalili za ugonjwa huo zinapojitokeza, huwa katika hatua za mwisho za ugonjwa ambapo ini huwa limeshaharibiwa kiasi kikubwa na hivyo tiba za magonjwa nyemelezi hutolewa kusaidia kuyapunguza makali, na wakati mwingine ini huwa limeshambuliwa na saratani na hivyo nafasi ya mgonjwa kuishi hupungua na kuwa chini ya kipindi cha mwaka mmoja.
#JAMBOLEO Wasomi wamesema matamko ya mawaziri wa Elimu nchini ndio sababu ya kudidimia kwa Elimu kutokana na kupingana na Sheria ya Elimu pic.twitter.com/FcmZHxyMzK
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
#HABARILEO Viongozi wa kidini wameanza kufanya maombi maalumu kwa ajili ya wakazi wa Kizwite, Sumbawanga wanaodai kuchapwa VIBOKO usiku pic.twitter.com/L70sjmm3dQ
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
#HABARILEO Wanafunzi 526,653 sawa na 94.8% ya waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza pic.twitter.com/edNKme0eyc
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
#HABARILEO Wizara ya Elimu imesema haijazuia wenye Stashahada wenye sifa kujiunga vyuo vikuu badala yake imezuia waliofeli kidato cha 4 na 6 pic.twitter.com/WUMXF575PB
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
#HABARILEO Kocha Pep Guardiola anaamini kuwa Man U bado wako ktk mbio za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu England dhidi ya Man City, Chelsea, Liva pic.twitter.com/ICMclOtkRw
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
#UHURU Naibu Waziri Luhaga Mpina amesema mawaziri wa Rais JPM sio waoga na wanamshauri Rais kama inavyodaiwa na baadhi ya wapinzani pic.twitter.com/F07b1Ix7Y3
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
#UHURU Wananchi wametakiwa kuwapa Elimu watoto wao ili kupunguza migogoro kwa kuwa watatumia Elimu yao badala ya kusubiri mzazi afe warithi pic.twitter.com/4IIGKCfuak
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
#MWANANCHI Watumishi wanne wa Taasisi ya TAKUKURU waliosimamishwa baada ya kusafiri nje ya nchi kinyume na agizo la Rais wamerejeshwa kazini pic.twitter.com/kFCjqV2VQp
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
#MWANANCHI Mwenyekiti wa CHAUMMA Hashim Rungwe amesema kinachooneshwa na Rais Magufuli ktk kazi zake ni tabia yake binafsi na si utendaji pic.twitter.com/VKmNd4osLh
— millardayo (@millardayo) November 29, 2016
VIDEO: Alice Tupa kutoka Ayo TV amekuchambulia stori kubwa zote za Magazeti yote ya leo November 29, 2016 na tayari nimekuwekea hapa.