Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu kufariki kwa aliyewahi kuwa mke wa Raisi wa kwanza wa Afrika Kusini Winnie Mandela, Mbunge wa Muleba kusini Prof Anna Tibaijuka amekutana na Ayo TV kwenye exclusive interview ambapo ameonesha kukerwa na baadhi baadhi na tuhuma alizowahi kupewa mwanaharakati huyo ikiwemo kuua.
“Sasa hivi Winnie Mandela ndio anatambuliwa kwamba aliweka mchango mkubwa, kwanini wakati wa uhai wake alifanyiwa kila hila na kusingiziwa? Mimi kusingiziwa nakujua…! wanasema aisifiaye mvua imemnyea”
“Winnie Mandela alisingiziwa mambo makubwa kwamba aliua mototo lakini leo wanasema ilikuwa dili tu kumchafua Yule mama. Hii inatupa moyo hata sisi ambao tumesingiziwa mambo kwamba kuna siku watu watakuja kujua ukweli uko wapi na watabaki kushangaa ” –Prof Anna Tibaijuka
Utani wa Spika Job Ndugai baada ya Yanga kupewa kipigo na Simba