Kampuni ya Taifa ya Mafuta Uganda imeanza kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam Tanzania kuelekea Uganda baada ya Mamlaka za Kenya kukataa kuruhusu mafuta hayo kusafirishwa kupitia bomba la mafuta nchini humo.
Inaelezwa kuwa Uganda wana mpango wa kusafirisha karibia lita milioni 36 kwa mwezi sawa na malori ya mafuta 1,028 kupitia Dar es Salaam ambayo kwa kawaida huwa yanasafirishwa kupitia mfumo wa KPC.
Hatua ya kwanza itakuwa ni kusafirisha lita milioni 18 (Malori 520) ambayo itaanza wiki hii kutokea Dar es Salaam na kutarajiwa kuwasili Kampala siku chache zijazo.
Wauzaji wa mafuta Uganda wameipokea hatua hiyo kwa mikono miwili sababu itawasaidia kusambaza mafuta hayo kutokana na uhitaji waliokuwa wanataka kutoka Kenya.
Serikali ya Kenya sasa itapoteza mapato mengi kutokana na kutoruhusu bomba lao la mafuta kutumika kusafirishia mafuta hayo.