Hii leo nchini Uganda, kutasikilizwa maombi matatu dhidi ya sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja iliyopitishwa mapema mwaka huu na Rais Yoweri Museveni iliyopelekea watu wengi kusema wanahofia maisha yao.
Mnamo Agosti, mwanamume mwenye umri wa miaka 20 alikuwa mtu wa kwanza kufunguliwa mashitaka kwa kosa la ‘mapenzi ya jinsia moja kulikokithiri’ na akuwa katika hatari ya kupata hukumu ya kifo.
Ripoti ya hivi majuzi ilisema kumekuwa na ukiukwaji zaidi ya mia tatu wa haki za binadamu uliorekodiwa mwaka huu dhidi ya raia wa LGBTQ+, huku makundi ya kutetea haki za binadamu yakisema watu wameteswa, kupigwa, kukamatwa, na kufukuzwa kwa sababu ya mwelekeo wao wa kijinsia na utambulisho wa kijinsia.
Msemaji wa serikali alisema matokeo ya utafiti huo yameghushiwa na kupendekeza ripoti hiyo iliandikwa ili kupata pesa.