Mamlaka ya Uganda jana imesema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameathiriwa na maporomoko ya ardhi kwenye dampo la Kiteezi huko Kawempe, Kampala, na idadi ya vifo imefikia 24.
Waziri wa Nchi anayeshughulikia Misaada, Maandalizi ya Maafa na Wakimbizi Lillian Aber, ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa maporomoko hayo yalisababisha uharibifu na kuathiri jamii katika vijiji vitatu vya Lusanja, Kitetika na Kiteezi.
Amesema watu walioathiriwa wanakadiriwa kuwa zaidi ya 1,000 kutoka vijiji vyote vitatu, na familia 56 zilizokimbia makazi yao zilisajiliwa katika makazi ya muda na Ofisi ya Waziri Mkuu na Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Uganda.