Maafisa wa Uganda wanajitahidi kuhakikisha kuwa Waganda 59 waliozuiliwa katika vituo vitano katika mji mkuu wa Uturuki,
Ankara, wameachiliwa.
57 kati yao walikamatwa kwa kukawia viza zao katika msako mkali wa serikali dhidi ya wahamiaji wasio na vibali, ambao
umeshuhudia zaidi ya watu 10,000 wakiripotiwa kufukuzwa mwezi Julai.
‘Tunafanya kila tuwezalo kuwasaidia kwa sababu Waganda wengi, hasa wale waliokuwa kazini [visa] walikuwa wametuma
maombi ya kuongezewa muda wa kukaa na walikamatwa wakati wa mchakato wa kuongezwa’ balozi wa Uganda nchini
Uturuki, Nusura Tiperu, aliliambia gazeti la kibinafsi la Daily Monitor la Uganda.
Waganda wengine wawili wanakabiliwa na tuhuma za ulanguzi wa binadamu na wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya
Uturuki.