Masaa kadhaa baada ya mtu mmoja ambaye ni raia wa Uganda kupigwa risasi na kuuawa na polisi mjini California siku ya Jumatano, Serikali ya nchi hiyo imetoa agizo kwa Ubalozi wake jijini Washington DC nchini Marekani, kuchukuza na kutoa maelezo ya kina mazingira yaliyosababisha kifo cha raia wake Alfred Olango.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Uganda Margaret Kafeero ameliambia Gazeti la kila siku nchini Uganda la Daily Moniter kuwa, Serikali imemtaka Balozi wa Uganda kufanya uchunguzi wake, ili kubaini kilichosababisha Olango kupigwa risasi.
>>>>Tumemwagiza Balozi wetu mjini Washington DC kutafuta ukweli wa jambo hili kwa sababu kile tunachokifahamu tu ni kuwa, raia wetu amepigwa risasi na kuuawa:- Amesema Waziri Kafeero.
Polisi nchini Marekani wamekiri kuwa, raia huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka 30 alipigwa risasi baada ya kuonekana alitoa kitu mfukoni katika makabiliano na maafisa wa polisi, hata hivyo, polisi wamesema mtu huyo hakuwa amebeba silaha wakati wa tukio hilo
Baada ya tukio hilo, Wamarekani weusi na raia wengine weusi waljitokeza na kuanza kuandamana kulaani mauaji hayo na imebainika kuwa, Olango alikuwa ni mkimbizi kutoka nchini Uganda lakini pia alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya akili, suala ambalo pia huenda lilichangia makabiliano yake na polisi.
Polisi wamesisitiza kuwa, walimwagiza atoe mikono mifukoni mwa suruali yake lakini akatoa kitu ambacho kimebainika kuwa sigara ya kieletroniki, Marekani imeendelea kushuhudia vifo vya Wamarekani na wahamiaji haramu mikononi mwa polisi wazungu.
ULIPITWA NA HII YA BINTI ALIYETOROKA BAADA YA KULAZIMISHWA KUOLEWA? ITAZAME HAPA