Taarifa ikufikie kwamba Afrika Mashariki imeingia kwenye headlines za mapinduzi makubwa ya kiteknolojia kwa kutengeneza gari la aina tofauti na ile tuliyozoea barabarani.
Kwanini nimeyaita mapinduzi makubwa katika industry? tumezoea kutumia magari yanayotumia mafuta na baadhi yanayotumia gesi lakini hii mpya ni ya Uganda ambayo inatarajia kuzindua gari la kwanza kutengenezwa nchini humo ambalo linatumia umeme.
Ni hili kwenye picha na video kwenye hii post ambalo limetengenezwa kwa msaada wa Serikali ya Uganda.
Kiira Motor ambao ndio watengenezaji wamesema wanahitaji dola za kimarekani laki tatu na elfu 50 kama mtaji wa kuanza kuzalisha magari hayo na kuyatengeneza katika aina 19 tofauti ambapo wanataka kuanza kuyatoa mwaka 2018 huku lengo lao likiwa ni kutoa magari 300 kwa mwezi.
Pichaz zote na video ni kutoka kituo cha TV cha K24.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook