Leo July 26, 2020 Taarifa iliyotolewa na Mwanafamilia wakati wa Misa ya kumuaga Rais Mstaafu Hayati Benjamin William Mkapa imesema Sababu ya kifo chake ni Mshituko wa Moyo(cardiac arrest).
“Mzee wetu aliugua akaenda hospitali akachukuliwa vipimo akakutwa na malaria akalazwa, Alhamis mchana alikuwa vizuri, alikuwa anatazama taarifa ya habari, baada ya hapo aliinuka akataka kutoka akainamisha kichwa, mpaka walipo mpima alikua kaishafariki” Mwanafamilia ya Mkapa
“Nilidhani ni vizuri tuliseme kwa sababu kumeanza kuwa na maneno maneno kwenye mitandao, niwaombe na kuwasihi Watanzania wenzangu tumuenzi Mzee wetu aliyetangulia mbele ya haki kwa kuheshimu ukweli huo, kwamba hicho ndicho kilichosababisha kifo chake” Mwanafamilia ya Mkapa