Kufuatia changamoto inayoendelea visiwani Zanzibar ya kukosekana kwa mafuta na kusababisha foleni kwenye vituo Chama cha Act Wazalendo zanzibar kimeitaka mamlaka ya mafuta Zanzibar ZURA kuzungumza sababu zilizoifanya zazibar kukosa mafuta na sababu ya meli kuchelewa licha ya sababu walizozitaja mamlaka hiyo kua changamoto ya meli kuchelewa imepelekea mafuta kukosekana na kusababisha foleni kubwa kwenye sheli
Chama cha ACT wazalendo kwenye barua yao waliitoa wamedai kua– ACT Wazalendo, tunazo taarifa za kuaminika kwamba, mafuta yaliyoingia nchini ni lita milioni mbili tu, wakati nchi ina uhitaji wa matumizi ya mafuta lita laki mbili kwa siku, ni wazi kwamba kiwango hichi cha mafuta kilichoingia chini ni kidogo sana na hayana uwezo wa kuhimili hata kwa matumizi ya siku 10.
Utaratibu unaotumika kugawa mafuta kwa wamiliki wa vitu vya mafuta kwa kuwapatia Mafuta yasiyozidi lita 2000, ni wazi kwamba kunaonesha uwepo wa tatizo kubwa la mafuta.
Chama hicho kimeendelea kuitaka mamlaka hiyo ijitokeze na iyeleze sababu kwa wananchi zilizopelekea meli hiyo kuchelewa ,kadhia hiyo ya mafuta Zanzibar inasadikika ilianzia kutokea siku ya jumamosi kwa baadhi ya vituo na kisha kuendelea kwa sheli nyingine na kupelekea kuwepo kwa chagamoto kwa sheli nyingi zinazopatikana Zanzibar