Mchezaji wa klabu ya Chelsea Hakim Ziyech amenyimwa tena kuondoka kwenye klabu hiyo ya Premier League baada ya kufeli vipimo vyake vya kiafya katika klabu ya Al-Nassr.
Ziyech amevumilia wakati mgumu Stamford Bridge tangu ajiunge na The Blues kutoka Ajax na ana nia ya kufufua soka lake kwingineko.
Hapo awali alijaribu kuondoka Januari, lakini Chelsea walikosa hati katika uhamisho wake wa kwenda PSG .
Kwa mujibu wa Foot Mercato, klabu ya Al-Nassr ya Saudia ina wasiwasi juu ya tatizo la goti ambalo limebainika wakati wa kufanyiwa vipimo vya afya mchezaji huyo na sasa dili hilo liko hatarini.
Ziyech alitarajiwa kukamilisha uhamisho wa £8m ili kuungana na Cristiano Ronaldo lakini sasa huenda uhamisho huo ukafutiliwa mbali.
PSG waligundua tatizo kama hilo Januari lakini walifanya majaribio zaidi ili kukamilisha mpango huo, ambao uliishia kutotimia kadri muda ulivyopita.
Ziyech alitarajiwa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 17 kwenda Saudi msimu huu wa joto.
Kushindwa kwake kiafya kunamaanisha kwamba hatua hiyo sasa haitafanyika, huku Ziyech akiwa bado amekwama Stamford Bridge.
Matokeo ya vipimo hivyo yalipatikana siku hiyo hiyo Al-Nassr walikubaliana na Inter Milan kumnunua kiungo Marcelo Brozovic.