Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ofisi yake imepokea barua za watuhumiwa 467 wanaoomba kukiri makosa ya uhujumu uchumi na wapo tayari kurudisha fedha jumla ya Shilingi 107.8 Bilioni.
Pia DPP amemuomba Rais John Magufuli kuongeza siku tatu kwa ajili ya kuwapa nafasi watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali.