Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alitangaza hivi karibuni kurudisha Tsh. mil 40.4 alizopewa na mfanyabiashara James Rugemarila ambaye anahusishwa na tuhuma za ESCROW na kuibua mijadala katika jamii.
Hatua ya Ngeleja kurudisha fedha hizo imeibua mijadala mbalimbali katika jamii ambapo watu mbalimbali waikiwemo Wanasheria wamekuwa wakiizungumzia issue hiyo ambayo tayari baadhi ya wahusika wamefikishwa Mahakamani akiwemo Rugemarila na kusomewa mashtaka.
Miongoni mwa wanasheria hao ni Hashimu Mziray ambaye anasema alichokifanya Ngeleja ni udhaifu na anatakiwa kuomba radhi, kwani fedha hizo alizichukua muda mrefu na huenda alizifanyia uzalishaji ambapo kisheria halijakaa sawa.
Ayo TV na millardayo.com zimempata Mwanasheria Hashimu Mziray ambaye anaeleza zaidi.
Majibu ya Tundu Lissu kuhusu kumfuta uwanachama Waziri Mwakyembe!!!