Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza James Cleverly alisema Uingereza itashirikiana na washirika wake wa karibu kujua kilichotokea katika Hospitali ya Al-Ahli ya Gaza na kuwalinda raia wasio na hatia huko Gaza.
Katika chapisho kwenye X, mwanadiplomasia mkuu wa Uingereza aliandika: “Kuharibiwa kwa hospitali ya Al Ahli ni hasara kubwa ya maisha ya binadamu.”
“Uingereza imekuwa wazi. Ulinzi wa maisha ya raia lazima uwe wa kwanza. Uingereza itashirikiana na washirika wetu kujua nini kimetokea na kuwalinda raia wasio na hatia huko Gaza,” alisema.
Serikali ya Uingereza – pamoja na uongozi wa chama cha upinzani cha Labour – imeweka wazi kuwa inasimama nyuma ya Israeli katika mzozo wa sasa.