Serikali ya Uingereza imesema itaruhusu kufunguliwa tena kwa nyumba za ibada kwa Mtu mmojammoja ifikapo June 15 wakati Taifa hilo likijaribu kuharakisha kuondoa vizuizi vya vya corona ili kunusuru ajira.
Uingereza imepanga pia kufungua tena maduka ifikapo June 15 katika juhudi zake za kurejesha maisha ya kawaida tangu ilipoweka marufuku kali kuzuia kuenea virusi vya corona March 23,2020.
Tayari idadi ya watu waliofariki na ugonjwa wa COVID-19 nchini Uingereza imefikia zaidi ya 40,000 ikiwa nchi ya pili kwa idadi kubwa ya vifo Duniani baada ya Marekani.
RAIS MAGUFULI “CORONA IMEKOROMEA, MADAWA TUNAYO, TUENDELEE KUJIFUKIZA”