Rais Volodymyr Zelenskyy azuru nchini Uingereza jumatatu katika ziara yake ,huku mshirika mkubwa wa Kyiv akiahidi kuipatia Ukraine mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani katika juhudi za kubadilisha mkondo wa vita.
Zelenskyy alitua kwa helikopta katika eneo la Chequers, makao rasmi ya kiongozi huyo wa Uingereza, na kulakiwa na Waziri Mkuu Rishi Sunak hii ni safari ya pili ya Zelenskyy kwenda U.K. tangu Urusi ilipovamia Ukraine mnamo Februari 2022.
Hii ni nchi ya nne ya Ulaya Zelenskky kuzuru katika siku chache zilizopita. Anatafuta usaidizi zaidi huku Ukraine ikitayarisha shambulio lililotarajiwa kwa muda mrefu ili kutwaa tena eneo lililotekwa na Urusi.
Kiongozi wa Ukraine alifanya ziara bila kutangazwa mjini Paris Jumapili jioni kukutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, baada ya safari za Ujerumani na Italia, ambapo alikutana na viongozi wa nchi hizo na Papa Francis.
Ujumbe uliotumwa Jumatatu kwenye Channel rasmi ya Telegraph ya Zelenskyy ulisema: “Leo – London. Uingereza inaongoza linapokuja suala la kupanua uwezo wetu ardhini na angani. Ushirikiano huu utaendelea leo,nitakutana na rafiki yangu Rishi. Tutafanya mazungumzo ya kina ana kwa ana na katika wajumbe.”
Uingereza imekuwa mojawapo ya washirika wakuu wa kijeshi wa Ukraine, ikituma makombora ya masafa mafupi ya Kyiv na vifaru vya Challenger na kutoa mafunzo kwa wanajeshi 15,000 wa Ukraine katika ardhi ya Uingereza. Wiki iliyopita Uingereza ilitangaza kuwa imetuma makombora ya meli ya Ukraine Storm Shadow, ambayo yana umbali wa zaidi ya kilomita 250 (maili 150) – shehena ya kwanza ya silaha ambayo Kyiv imekuwa ikitafuta kwa muda mrefu kutoka kwa washirika wake.
Serikali ilisema Bw Sunak atathibitisha leo utoaji zaidi wa mamia ya makombora ya ulinzi wa anga na mifumo zaidi ya angani isiyo na rubani, ikijumuisha mamia ya ndege zisizo na rubani za masafa marefu zenye umbali wa zaidi ya kilomita 200.
chanzo:CNN