Michuano ya Mapinduzi Cup 2019 imeanza leo lakini kwa mwaka huu inashirikisha jumla ya timu 9, hiyo ni baada ya URA ya Uganda na Bandari ya Kenya kunyimwa ruhusa na mashirikisho yao ya soka kuja kushiriki michuano hiyo, huku kutoka Tanzania timu za Yanga, Simba na Azam FC ndio zinashiriki.
Meneja wa Simba Abbas Kuka tayari amewasili Unguja lakini timu inawasili asubuhi ya January 2 2019 ikitokea Dar es Salaam, Abbas amethibitisha kuwa licha ya Simba kukabiliwa na mchezo muhimu wa CAF Champions League dhidi ya JS Saouro ya Algeria January 12 lakini wataleta kikosi chao kamili cha wachezaji 27 ila wataondoka wachezaji 19 January 8 kwenda Dar es Salaam kwa ajili game dhidi ya JS Saouro.
VIDEO: Furaha ya ushindi Kocha wa Simba kashangilia hadi kavua shati