Leo Febr 03 2016 Bunge la 11 liliendelea mjini Dodoma na moja ya ripoti zilizonifikia ni hii ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alivyowasilisha ripoti ya matukio ya Ujambazi na yale ya Watu kujichukulia sheria mikononi.
Waziri Masauni anasema “Matukio ya ujambazi yanayohusisha uporaji wa fedha yalikuwa kama ifuatavyo, mwaka 2013 matukio 1266, 2014 matukio 1127, 2015 matukio 913, jumla ni matukio 3306 ambayo yalisababisha vifo 91 na majeruhi 189“
“Mikoa iliyoongoza ilikuwa ni Dar es salaam ilikuwa na matukio 733, ukifuatiwa na Mara matukio 375 na takwimu za matukio ya kujichukulia sheria mkononi zinasema ni jumla ya matukio 2100 yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi nchini”
Hapa nimekusogezea sauti ya Naibu Waziri Masauni, unaweza kuisikiliza yote.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.