Mwenyekiti wa Baraza la Diaspora Duniani(TDC Global)Norman Jasson amesema kuwa Watanzania waishio Nchi za nje (Diaspora)wapo kwenye mkakati wa kujenga Daraja lenye urefu wa takribani Kilomita 30.01 kutoka DSM hadi Zanzibar .
Kwa sasa wanasubiri Baraka za Serikali ili kuanza upembuzi yakinifu ili kujua gharama za ujenzi wa Daraja hilo, Daraja hilo litakuwa na njia 3, moja ni kupitisha magari yanayotoka DSM kwenda Zanzibar na njia ya pili ni magari yanayotoka Zanzibar kuja DSM na njia ya tatu ni kwa ajili ya watembea kwa miguu na waendesha baiskeli.
Mapendekezo matatu ya ujenzi wa Daraja hilo yametolewa ambayo ni kujenga Daraja la kupita ndani ya Bahari, pili Daraja la kupita juu na tatu ni daraja linaloelea majini ambalo ndilo lililopendekezwa na ujenzi wake ni rahisi maana hutengenezwa Nchi Kavu na kusafirishwa na Meli na kisha kuunganishwa.
Daraja la ndani ya maji halikuchaguliwa kwasababu ndani ya maji DSM badi Zanzibar kuna mkondo wa maji na maporomoko, Daraja la juu halikuchaguliwa kwasababu Bahari ya Hindi eneo hilo kuna kina kirefu, Daraja la kuelea limechaguliwa kwasababu ujenzi wake ni rahisi na gharama zake ni nafuu na garantii yake ni miaka 100.
WAZIRI JAFO AMUOMBA MAGUFULI AMPANDISHE CHEO DC JOKATE “UNANG’AA, NAMUOMBA JPM AMUONE SANA”