Balozi wa Tanzania nchini DRC Said Mshana, ameshiriki kikao cha nchi tatu cha Mawaziri wa Uchukuzi na kushuhudia utiaji saini mkataba wa usanifu na upembuzi yakinifu wa reli ya kisasa Gitega-Bujumbura-Uvira-Kindu kati ya CCTTFA kwa niaba ya serikali za Burundi na DRC na mkandarasi CPS Zutari
Hii ni muendelezo wa juhudi za serikali tatu za Tanzania-Burundi na DRC katika ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR)ambapo kipande cha Tanzania mpaka Burundi kipo katika hatua mbalimbali. Tukio hili lilihudhuriwa na Mawaziri, Makatibu wakuu, Mabalozi wa nchi zote tatu pamoja na wataalam
“Tunaamini kwamba Nchi za ushoroba wa kati zikijikita katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa kama hii,kutasaidia sana katika kufanikisha usafirishaji wa mizigo”amesema.
.