Taasisi moja mashuhuri ya utafiti nchini Ujerumani imemsimamisha profesa wa anthropolojia anayeiunga mkono Palestina, baada ya msomi huyo kukosoa mashambulizi yanayoendelea kufanywa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Kulingana na Press TV imeripoti habari hiyo na kueleza kuwa, Taasisi ya Utafiti ya Max Planck Society imevunja mkataba wake na mwanaakademia Ghassan Hage, kutokana na machapisho yake kadhaa katika mitandao ya kijamii ambayo kuwa hayaendani na ‘thamani za kijamii’.
Taasisi hiyo mashuhuri ya utafiti ya Ujerumani imedai katika taarifa kuwa: Ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya Uislamu, chuki dhidi ya Mayahudi, kubaguana, uchochezi na chuki hazina nafasi katika taasisi ya Max Planck Society.
Profesa huyo wa Chuo Kikuu cha Melbourne mwenye uraia pacha wa Lebanon na Australia amelaani vikali uamuzi wa Taasisi ya Utafiti ya Max Planck Society wa kumfukuza kazi, kutokana na hatua yake ya kutumia uhuru wake wa kujieleza kukosoa jinai za Israel huko Gaza.