Leo April 2018 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Ashatu Kijaji amewasilisha bungeni, kauli ya serikali kuhusu hoja ya kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali Shilingi Trilioni 1.5
“Hakuna fedha taslim TRILIONI 1.5 zilizotumika pasi na kuwa na maelezo ya matumizi yake, wanaodai kuwa fedha hizo zilitumika bila maelezo, hawalitakii mema taifa na serikali ya awamu ya tano.”– Naibu Waziri wa Fedha, Dr Ashatu Kijaji
“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ipo makini na haiwezi kuruhusu kwa namna yoyote ile upotevu wa fedha za umma. Tunahakikisha kila mapato yanayokusanywa yanatumika ipasavyo kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania”– Naibu Waziri Dr. Ashatu Kijaji
MAGAZETI LIVE: CAG aibua watumishi hewa, Harusi ya Alikiba yatikisa Afrika Mashariki