NI kufuatia kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais ambae alifariki leo Jumatano saa 5:00 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.Sasa Zitto Kabwe ameitisha Mkutano wa waandishi wa habari na kuzungumza kufuatia kifo hicho’
‘Mwenyekiti wetu wa Chama Maalim Seif ametutoka, hakuna maneno ambayo tunaweza kuyaeleza kwa Wanachama, Wazanzibar na Watanzania kuhusiana na uchungu wa taarifa hii’- Zitto Kabwe,
‘Kwa mujibu wa taarifa ya Madaktari, leo alikuwa anaonesha matumaini ya kupata nafuu, ilipofika saa tano akafariki, Maalim Seif alitulea kiuongozi, alikuwa na nia ya kuiona Tanzania yenye Demokrasia na Zanzibar ya maridhiano’-Zitto Kabwe
‘Taarifa za mipango ya mazishi tutazitoa baada ya mashauriano kati yetu Chama, Serikali na Familia, sisi kama Chama tutatoa ushirikiano kwa Serikali ili kuhakikisha tunampumzisha Mzee wetu’ – Zitto Kabwe
‘Nawaomba Wazanzibar na Watanzania kuwa Watulivu katika kipindi hiki tulichoondokewa na Mwamba wa Demokrasia Maalim Seif’– Zitto Kabwe