Jana August 24 2016 viongozi wa dini waliendelea na kikao chao cha kutafuta maridhiano ambapo kikao hicho kilijadili mvutano baina ya wabunge wanaompinga Naibu spika, Dk Tulia Ackson na operesheni UKUTA. Viongozi hao wa dini walitoa rai kwa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ‘UKAWA’ kurudi bungeni katika bunge lijalo.
Leo August 25 2016 vyama vya upinzani vyenye wabunge bungeni vimekutana na waandishi wa habari ambapo akizungumza kwa niaba yao mbunge wa Vunjo na mwenyekiti wa chama cha NCCR-MAGEUZI wamesema wamesikia ombi walilopewa jana na viongozi wa dini la kuwataka kurudi bungeni Bunge lijalo kwahiyo watakaa kujadili ombi hilo la viongozi wa dini……
>>>‘tumeipokea rai yao vizuri na tunawahakikishia tutakutana sisi wabunge wote wa vyama vinne tuliotoka bungeni, tuitafakari kwa kina rai yao ya viongozi wetu wa dini au kwa lugha nyingine agizo lao, mkubwa akikuomba ni kwamba amekuagiza ili tuone ni namna gani tutakavyolitumia na tufikirie chanya namna gani tutakavyorudi bungeni kwa maslahi mapana ya nchi’
ULIKOSA HII YA UKAWA KUZUNGUMZIA MAUAJI YA POLISI DAR KUHUSISHWA NA SIASA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI