Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora Lazaro H Msasalaga, ametoa ufafanuzi juu ya ukaguzi wa magari yaliyotumika yanayotoka nje kwa Makampuni ya Uagizaji Magari na Mawakala wa Forodha katika mkutano uliofanyika TBS Makao Makuu.
Msasalaga alieleza mabadiliko haya ya ukaguzi wa magari yametokea baada ya kujihakikishia kuwa kama nchi sasa tunao uwezo wa kupima magari tofauti na awali ambapo magari yalikuwa yanakaguliwa na Mawakala wa TBS katika nchi husika kabla ya kuingia nchini.
Alieleza kuwa kupitia mabadiliko haya faida mbali mbali zitapatikana ikiwemo ongezeko la ajira kwa wananchi pamoja na kuongezeka kwa mapato ya nchi na kuwahakikishia wadau wa uagizaji magari na Mawakala wa Forodha kuwa wasiogope kwani TBS kwa kushirikiana na taasisi nyingine imejidhatiti kutoa huduma hiyo kwa ufanisi mkubwa.