Ni Julai 28, 2023 ambapo Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa anazungumza muda huu kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa Clouds FM 88.5.
“Bahati mbaya wapo watu ambao sio waadilifu ambao wanavuna kutokana na changamoto zetu za bandari, kwa maslahi yao binafsi [zaidi ya Tsh. Bilioni 200 kwa mwezi]. Ukichunguza vizuri utagundua kelele nyingi zinaletwa na hawa wanufaika na washirika wao, bila kujali kwamba halii hii inawabebesha mzigo wafanyabiashara ambao mwisho wa siku wanaihamishia hii gharama kwa wananchi kwa kuongeza bei za bidhaa. Matokeo yake ni mfumuko wa bei ambao unawaumiza wananchi wa kawaida. Hatuwezi kukubali hili liendelee.” Jerry Silaa Mbunge wa Ukonga