Dkt Tumaini Msowoya, Mjumbe wa Bodi ya Shule ya Ufundi ya Ifunda amepata nafasi ya kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha sita aliwasisitiza kuongeza bidii, nidhamu na kuwasikiliza walimu wakati huu wa maandalizi ya mitihani yao ya mwisho.
Amesema bado wanafunzi ambao wanadhani hawakuwa wamejiandaa vizuri wanayo nafasi ya kutengeneza daraja la kwanza katika mitihani yao.
Dkt Msowoya amesema bidii ya kujisomea, nidhamu, kuwasikiliza walimu, kujiamini, kuachana na makundi mabaya na kumcha Mungu vitawasaidia kutimiza ndoto zao.
“Mna siku chache tu mmalize mitihani yetu, nawatakia heri na ni Imani yangu kila mwanafumzi atafaulu. Kama ulikuwa daraja la pili au tatu, naweza kutumia siku hizi chache kujiandaa na ukarudi daraja la kwanza,” amesema na kuongeza;
“Ukifaulu ni furaha kwa wazazi, walezi, shule, walimu, wanafunzi wenzako na Taifa zima. Inawezekana,”
Shule ya Ufundi ya Ifunda imekuwa ikitenga muda kwa baadhi ya wajumbe wa bodi chini ya Mwenyekiti wake, Mr Mark kuzungumza na wanafunzi ili kuwaongezea ujasiri, kujiamini na kujitambua.