Wakati Serikali ikiendelea kuboresha huduma za maji Kwa kujenga miundombinu maeneo Mbalimbali bado wapo baadhi ya watu wamekua wakirudisha nyuma jitihada hizo Kwa kuiba Dira za maji (Mita) pamoja na maunganisho yake na kuuza chuma chakavu.
Kaimu mkurugenzi MORUWASA Lyang’onjo Kiguhe amesema Kwa kipindi cha mwezi januari pekee mwaka huu Dira za maji 52 zimeibwa katika maeneo Mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro na kuleta hasara zaidi ya milioni tano Kwa mamlaka hiyo.
“Hali ya usalama kwa miundombinu ya maji Manispaa ya Morogoro sio nzuri Kwani watu wanaendelea kuhujumu miundombinu ya maji Kwa kuiba Dira za maji ambapo mwezi januari zimeibwa Dira 52 ”
Kutokana na chamgamoto hiyo mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira Morogoro ( MORUWASA) wamekutana na wanunuzi wa chumachakavu Manispaa ya Morogoro ili Kuwapa elimu namna ya kutambua Mali za mamlaka hiyo na kushiriki kuwakamata wezi wa miundombinu hiyo.
Mwanasheria wa MORUWASA Tumain Kimaro anasema Kwa Mtu yoyote atakayekamatwa Kwa kuharibu au kuiba vifaa vya maji na Uchepushaji atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na anaweza kulipa faini kuanzia laki tano Hadi milioni 50 au kifungo cha miaka mitano.
Anasema mamlaka hiyo Kwa sasa imedhamiria katika kulinda Rasilimali za maji hivyo mpango ni kuendelea kusimamia Sheria zilizopo ili kuisaidia kuondokana na hasara zisizo za lazma
Majuto John mmoja wa wauza Chuma chakavu Morogoro anasema awali walikua hawafahamu madhara ya kununua vitu hovyo lakin kupitia elimu waliyopatiwa watakua walinzi kwa Kutoa taarifa kwenye uongozi pindi watakapo letewa vifaa hivyo na wezi.
Naye afisa mnadhimu wa polisi Mkoa Morogoro ACP Hassan Omary amesema jeshi la polisi litaendelea kushirikiana wananchi ili kuinua watu wanaofanya uharibifu na wizi miundombinu ya maji.
Anasema hadi sasa wamewakamata watu Saba ambapo Kati Yao watano wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kuiba miundombinu ya maji na Kutoa wito kwa jamii kuacha Kufanya vitendo hivyo
MORUWASA wamesema mtu atakayemkamata mwizi au anayeharibu miundombinu ya maji atapewa shilingi laki tano papo hapo kama zawadi na Kutoa wito Kwa wamiliki wa nyumba kuimalisha ulinzi Kwa jamii kulinda Dira hizi.
.