Kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu kuwagonga wanyama katika hifadhi ya taifa ya mikumi imeelezwa kwamba mnyama mwenye gharama kubwa zaidi ukimgonga ni tembo ambaye mtu atatakiwa kulipa dollar elfu 20 sawa na million 50
Huka Mwankusye mhasibu wa hifadhi ya mikumi amesema kutokana na tatizo hilo kuwa sugu wamekuwa wakiendelea kutoa elimu ikiwa ni pamoja na kupunguza mwendokasi hifadhini huku kwa kipindi cha miaka mitatu faini waliotozwa jumla ya zaidi ya millioni 280 kama faini
“Wanyama wengine wenye faini kubwa,ukimgonga simba nj dolla 7500 ukibadilisha inaenda zaidi ya millioni 18,Nyati mmoja ni dollar za kimarekani 2500 ambayo ni zaidi ya million 6,nyani unampomgonga unatozwa dollar 110 ambayo ni zaidi ya zaidi ya laki mbili”
Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Mikumi Agustino Masesa amesema kwamba hivi sasa zaidi ya ndege 10 hutua kila siku hifadhini zikiwa na watalii ambapo kwa mwaka mapato ya hifadhi hiyo ni zaidi ya billion 4 kwa mwaka