Mkuu wa Wilaya ya Iringa Veronica Kessy amewataka wanannchi wa Mkoa wa Iringa kuendelea Kujikinga na maambukizi ya Virusi Vya ukimwi na huku akikumbusha takwimu za maambukizi ya ugonjwa huo kwa mkoa huu bado ni makubwa .
Kessy ameyasema hayo wakati alipo hitimisha kilele cha kampeni za kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika mankspaa ya Iringa ambapo amesema kulingana na takwimu zilizotolewa mwezi disemba mwaka huu katika maashimisho ya ukimwi mkoa wa Iringa uko nafasi ya pili maambukizi sawa na asilimia 11 ukiongizwa na mkoa wa Njombe
“ Niwasisitize wanannchi wa mkoa wa Iringa ukimwi bado uko , takwimu zilozotolewa bado Iringa ina maambukizi makubwa ukiongozwa na mkoa wa Njombe hivyo tuendelee kupima na kuchukua tahadhari “
Hatahivyo Afisa ustawi wa Jamii kutoka manispaa ya Iringa Tiniel Mmbaga amesema tatizo la ukatili wa kijinsia bado liko kwasababu kwa kipindi cha miezi tisa matukio zaidi ya 432 yaliripotiwa huku ya watoto pekee yakiwa 208.