Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko amewataka Viongozi wajizuie kufanya maamuzi au kusema lolote wakiwa na hasira ili kuepusha kuzua taharuki, kujiletea madhara na hata wakati mwingine kumuonea Mtu ambaye hana kosa lolote.
Biteko amesema hayo Jijini Dodoma katika Warsha ya Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhusu Usimamizi na Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai iliyofanyika Jijini Dodoma.
“Jizuie kufanya jambo lolote au kusema lolote wakati una hasira, mambo mawili unapaswa kuyaepuka sana ukifurahi usiahidi utaahidi usichoweza, ukikasirika usilaani, utalaani Mtu ambaye kumbe kosa sio lake”
“Alituambia Mtu mmoja alikuwa kwenye kikao Binti mmoja alikuwa kwenye simu, anaongea wala hamuangalii yupo na simu, baadaye akamwambia ‘simama juu hivi kwanini unanidharau?, Mimi naongea uko bize na simu unachatichati’ akamwambia ‘Boss nisamehe naandika notisi za hiki unachosema hizi hapa!’ akamwona wa maana zaidi kuliko wengi waliokuwa wanamuangalia hawaandiki lakini je angemwambia kamata huyu weka ndani si ungemweka ndani akaenda na notisi kesho anakuja kukuambia nilikuwa nafanya kazi yako Boss”
“Ukikasirika usilaani , ukikasirika jizuie kusema, unaweza ukakasirika ukatamka jambo kubwa kwa Mtu ambaye kumbe mahali pa coma kuna kituo kikubwa basi ndio tofauti hamna kitu kikubwa, tena ukigundua unataka kukasirika angalia aliye chini yako mwambie DAS naomba hili jambo mulifuatilie halafu nyamaza, utabaki kuwa DC, DED na yule Mpuuzi atabaki na upuuzi wake na baadaye atachukukuliwa hatua tena smoothly bila wewe kupata madhara”