Mara nyingi Wataalam wa masuala ya Mazingira wamekuwa wakisisitiza kuhusu watu kutambua athari zinazotokana na mifuko ya Plastiki, na hii ishu iliwahi kujadiliwa Bungeni, Wabunge wamesikika wakilalamikia udhibiti wa Mifuko inayotengenezwa na kuingizwa TZ huku ikichangia athari za Kimazingira.
Uingereza hawako kwenye mjadala huo tena, kilichotengenezwa ni Sheria mpya ambayo imependekeza kwamba kila mfuko wa plastiki utauzwa kuanzia Pound 5 ambazo kwa TZ ni kama Tshs. 16,400/=… Uingereza wanachoamini ni kwamba bei ya Mifuko ikiwa juu kiasi hicho, watumiaji wa mifuko hiyo watakuwa wachache na haitozagaa tena mitaani !!
Tafiti za mwaka 2014 zilionesha jumla ya mifuko ya Plastiki Bilioni 7.6 ilitolewa kwa wateja kutoka kwenye Supermarkets za Uingereza, hiyo ni sawa na kila mtu mmoja alipatiwa jumla ya mifuko 140.
Wapo wanaoamini utaratibu huu mpya utasaidia watu kukumbuka kubeba mifuko yao kutoka nyumbani wanapoenda Supermarket ili kuokoa Tshs. 16,400/= ambayo wangeilipia kwa kununua mfuko mmoja tu wa kuwekea bidhaa ulizonunua.
Kuna kipande cha video pia ambapo wako walioongelea kuhusu ujio wa hiyo Sheria mpya Uingereza.
https://www.youtube.com/watch?v=RVOI806mjbQ
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE