Ukraine imekosoa vikali wito wa Papa Francis kwa Kyiv kufanya mazungumzo ya kusitisha vita vyake na Urusi na kuwa na “ujasiri wa kuinua bendera nyeupe”.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine anasema “haitainua bendera nyingine yoyote” zaidi ya rangi za buluu na njano ya nchi hiyo.
Na Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky alitupilia mbali maoni hayo na kuutaja kama “upatanishi wa njia ya mtandaoni”.
Msemaji wa Vatikani baadaye alisema Papa alikuwa anazungumza juu ya kusitisha mapigano kwa njia ya mazungumzo, na sio kujisalimisha.
Msemaji wa Vatican baadaye alisema Papa alikuwa anazungumza juu ya kusitisha mapigano kwa njia ya mazungumzo, na sio kujisalimisha.
Mahojiano na shirika la utangazaji la Uswizi RSI, iliyorekodiwa mwezi Februari, yamepangwa kurushwa tarehe 20 Machi kama sehemu ya kipindi cha kitamaduni.
Kulingana na nakala iliyonukuliwa na shirika la habari la Reuters, Papa aliombwa kutoa maoni yake juu ya mjadala kati ya wale wanaotaka Ukraine kutafuta suluhu na Urusi – au kupeperusha “bendera nyeupe”, kama mhojiwa alivyosema – na wale wanaobisha kuwa kufanya hivyo kungehalalisha uchokozi.
Papa alinukuliwa akisema: “Aliye na nguvu zaidi ni yule anayeangalia hali, kuwafikiria watu na kuwa na ujasiri wa kupeperusha bendera nyeupe, na kufanya mazungumzo.”
“Unapoona umeshindwa, mambo hayaendi sawa, lazima uwe na ujasiri wa kujadili,” aliongeza.
Wakati wa hotuba yake ya video ya kila siku Jumapili, Rais Zelensky hakumrejelea Papa moja kwa moja, lakini badala yake alisifu kazi ya makasisi wa Ukraine kwenye mstari wa mbele.