Ukraine imewatambua watu 511 wanaoshukiwa kufanya uhalifu wa kivita tangu uvamizi wa Urusi Februari 2022 na tayari imetoa hatia 81, mwendesha mashtaka mkuu wake alisema mjini Kyiv siku ya Alhamisi.
Andriy Kostin alikuwa akizungumza katika mkutano wa uhalifu wa kivita pamoja na waendesha mashtaka wakuu wa Poland, Lithuania, Romania na Rais wa kitengo cha haki cha EU, Eurojust.
Katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wao, waendesha mashtaka walitangaza kutiwa saini kwa nyongeza ya miaka miwili ya kazi ya Timu ya Pamoja ya Upelelezi, mpango wa nchi tano za Umoja wa Ulaya kuchunguza uhalifu wa kivita katika mzozo huo.