Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kwamba kushindwa Urusi nchini Ukraine “haiwezekani kamwe”, lakini akasisitiza hataki kupanua vita katika nchi jirani kama vile Poland na Latvia.
Putin ameyasema hayo katika mahojiano na mtangazaji wa zamani wa Fox News, Tucker Carlson, na alirudia madai yake kwamba kuivamia Ukraine ni muhimu ili kuizuia nchi hiyo kuitishia Urusi kwa kujiunga na NATO, alikanusha kuwa alikuwa na malengo ya kumiliki ardhi kote Ulaya, na alisisitiza kuwa atatuma wanajeshi pekee katika nchi jirani ikiwa itashambuliwa kwanza.
“Nitakuambia kile tunachosema juu ya suala hili na kile tunachowasilisha kwa uongozi wa Marekani,” Putin alisema. “Ikiwa kweli unataka kuacha mapigano, unahitaji kuacha kusambaza silaha.
Itaisha ndani ya wiki chache, ndivyo hivyo, na kisha tunaweza kukubaliana kwa masharti fulani. Kabla ya kufanya hivyo,hakuna maswali.”
Putin alisema “hajawahi kukataa” kufanya mazungumzo ya amani na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy lakini Moscow bado haijafikia malengo yake nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na “de-Nazification”, akimaanisha madai yake kwamba Kyiv inafanya mauaji ya kimbari dhidi ya Warusi wa kabila.
“Na vita vya kimataifa vitaleta ubinadamu wote kwenye ukingo wa uharibifu. Ni dhahiri.”