Waziri wa Ulinzi wa Ukraine ameitetea hoja yake ya kuwavalisha Wanajeshi wa Nchi hiyo viatu virefu (high heels) lakini akaongeza kwamba watarudi mezani kuangalia namna ya kuyarekebisha maamuzi yake aliyotangaza wiki iliyopita na kuzua gumzo.
Waziri huyo alitangaza kwamba Wanajeshi hao wa kike watavaa viatu hivyo kwenye sherehe za miaka 30 ya uhuru wa Ukraine August 24 2021 lakini muda mfupi baada ya kutangaza maamuzi hayo baadhi ya Wabunge wa Ukraine walikosoa na kusema hata kiafya sio salama kwa Wanajeshi hao.
Kwa upande mwingine Jeshi la Ukraine limeanza kufanyia kazi agizo la Wanajeshi hao kuvaa high heels ambapo Major Eugene Balabushka amenukuliwa akisema Wanajeshi hao wa kike wamekua wakifanya mazoezi mara mbili kwa siku wakiwa wamevaa viatu hivyo tayari kabisa kwa kupiga navyo gwaride August 24 na mazoezi yanaendelea vizuri.
Ukraine ina Wanajeshi Wanawake wapatao elfu hamsini na saba (57,000) ambapo baada ya baadhi ya Watu kuukosoa uamuzi wa kuwavalisha high heels, Waziri wa Ulinzi aliitetea hoja yake kwa kupost picha mbalimbali za Wanawake wa majeshi mengine duniani wakiwa wamevaa high heels.