Watu wa kujitolea hawatoshi huku nchi inahitaji kila mara kuchukua nafasi ya makumi ya maelfu ambao wameuawa au kujeruhiwa,watu wengi zaidi wamechoka, baada ya miezi 18 kupigana na uvamizi kamili wa Urusi.
Wanaume wengine ingawa hawataki kupigana maelfu wameondoka nchini, wakati mwingine baada ya kuwahonga maafisa, na wengine kutafuta njia za kuwakwepa maafisa wa kuajiri, ambao nao wameshutumiwa kwa mbinu nzito zinazoendelea.
“Mfumo umepitwa na wakati,” anasema Yehor. Alimwona baba yake akiugua shida za afya ya akili baada ya kupigana na Jeshi la Soviet huko Afghanistan.
Ndio maana hataki kupigana. Ameombwa kwamba tusitumie jina lake halisi kulinda utambulisho wake.
Kwa kawaida, kabla ya uvamizi wa Urusi, wanaume ambao hawakutaka kufanya utumishi wa kijeshi wangepewa njia mbadala – kama vile kufanya kazi katika kilimo au huduma za kijamii.
Chaguo hilo lilitoweka na kuanza kwa sheria ya kijeshi mwaka jana, lakini Yehor anadhani bado inapaswa kupatikana.
“Kila hali ni ya mtu binafsi,” abisha Yehor. “Ukweli kwamba imeandikwa katika katiba kwamba raia wote wanaume wanapaswa kupigana, kwa maoni yangu, sio kulingana na maadili ya leo.”
Jinsi Kyiv inavyowaandikisha wanaume imeshutumiwa kuwa wafisadi katika msingi wake.
Rais Volodymyr Zelensky amemfuta kazi kila mkuu wa kanda ya kuajiri nchini Ukraine baada ya madai mengi dhidi ya maafisa katika mfumo huo, ikiwa ni pamoja na kupokea rushwa na vitisho.