Jeshi la Ukraine lilisema Jumatano kwamba lilidungua ndege 38 kati ya 63 za anga ambazo vikosi vya Urusi vilianzisha katika mashambulizi ya usiku.
Kikosi cha anga cha Ukraine kilisema kilinasa ndege hizo zisizo na rubani katika maeneo ya Cherkasy, Chernihiv, Kirovohrad, Kyiv, Mykolaiv, Odesa, Sumy, Zhytomyr na Zaporizhzhia.
Vitaliy Kim, gavana wa Mykolaiv, alisema kwenye Telegram kwamba shambulio la Urusi liliharibu miundombinu ya nishati, lakini haikuumiza mtu yeyote.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema Jumatano iliharibu ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine katika eneo la Kursk na ndege nyingine isiyo na rubani juu ya Oryol.
Maafisa wa Urusi walisema hakuna ripoti za uharibifu au majeruhi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumanne kwamba vikosi vya nchi yake vimepigana na wanajeshi wa Korea Kaskazini ambao walitumwa Urusi kusaidia katika vita vyake dhidi ya Ukraine.
“Mapigano ya kwanza na wanajeshi wa Korea Kaskazini yanafungua ukurasa mpya wa ukosefu wa utulivu duniani,” Zelenskyy alisema Jumanne katika hotuba yake ya kila siku – kukiri kwake kwa mara ya kwanza mapigano kati ya vikosi hivyo viwili.
Rustem Umerov, Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, pia amethibitisha kuwasili kwa vikosi vya Korea Kaskazini. Katika mahojiano na shirika la utangazaji la umma la Korea Kusini KBS, alisema vikosi vya Ukraine na Korea Kaskazini vimeshiriki katika mapigano “ndogo”.