Baada ya habari mbalimbali kuandikwa kwamba Mbunge wa Mbogwe, Nicodamus Maganga ameshikwa na maradhi ya akili na vichwa vya habari kama “Taharuki Mbunge Augua Uchizi” na kwamba Bunge limetuma Ambulance ili apelekwe Hospitalini lakini Baba yake Mzazi amezuia ili atibiwe kwanza kienyeji, Katibu wa Mbunge huyo ameongea na AyoTV.
Katibu huyu amesema Mbunge Maganga ni mzima wa afya kabisa na kuwataka Watu wazipuuze taarifa zinazosambaa “Mbunge ni mzima wa afya, alipatwapatwa na malaria akapumzika kama siku mbili lakini kwa sasa anaendelea vizuri na hivi karibuni ataendelea na majukumu, muda si mrefu ataanza kupatikana hata kwenye simu, Malaria inatibika tu nyumbani”