Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ‘LHRC’ leo August 30, 2017 kimezindua ripoti mpya ya Haki za Binadamu na Biashara ambayo imeonesha ukuaji wa 3% kwa wafanyakazi waliopewa mikataba ya ajira na waajiri wao ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa zipo changamoto ya zaidi ya 30% ya wafanyakazi wengi kutokufahamu haki yao ya kutibiwa na mwajiri wao endapo wataumia wakiwa kazini vivyo hivyo waajiriwa wengi pia hawajajiunga na mifuko ya kusaidia waajiriwa wao wanapoumia kazini.
Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Dr. Hellen Kijo-Bisimba amesema>>>”Kwenye upande wa ardhi asilimia 50 ya waliopewa ardhi kwa ajili ya uwekezaji hawajaitumia na asilimia kubwa ya walioitumia ardhi hiyo wameitumia kwa namna ambayo haijaruhusiwa.”
VIDEO: Mambo matatu Zitto kayasema kuhusu utafiti wa TWAWEZA leo
ULIPITWA? Mkuu mpya wa Polisi DSM kaanza kazi…