Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa mambo ya kibinadamu (OCHA) imesema mapigano kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) yaliyodumu kwa miezi kadhaa nchini Sudan yamelazimisha watu zaidi ya laki nne kukimbilia Sudan Kusini, na kati yao 13,130 waliwasili nchini humo kupitia jimbo la Upper Nile kuanzia tarehe 18 hadi tarehe 24 Novemba.
Asilimia 88 kati yao ni wasudan kusini wanaorejea kwao na nyingine asilimia 12 ni wakimbizi wa Sudan. Takwimu hizi imeonyesha mwelekeo wa kupungua kwa raia wa Sudan wanaoingia Sudan Kusini ikilinganishwa na wiki za hivi karibuni zilizopita.
Ofisi hiyo pia imesema chakula na fedha taslimu vimeshasambazwa kwa watu waliowasili hivi karibuni ili kukidhi mahitaji yao ya dharura ya chakula na lishe.