Umoja wa Mataifa, umeonya kuhusu mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa nchini Somalia, wakati huu watu 29 wakiripotiwa kufa na wengine zaidi ya laki 1 na elfu 13, wakipoteza makazi yao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunysha nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa, maelfu ya raia wengine katika taifa hilo la pembe ya Afrika wakilazimika kuhayama makazi yao kwa muda baada ya kuathiriwa na mafuriko hayo.
Mvua hiyo imeanza kushuhudiwa mwaka moja baada ya nchi hiyo kukabiliwa na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miongo mine.
Msimu wa mvua kubwa ya mwezi oktoba na mwezi Desemba imekuwa ikishuhudiwa katika eneo la Puntland na maeneo mengine.
Aidha ripoti hiyo ya Umoja wa mataifa imesema majimbo ya Kusini Magharibi na Jubbaland ndiyo yalioathirika zaidi, raia zaidi ya laki tano wakiathirika.
Mapema mwaka huu, zaidi ya watu laki mbili walipoteza makazi yao katika mkoa wa kati wa Somalia baada ya mto Shabelle kuvunja kingo zake.