Unaambiwa kuna sheria mpya inatarajiwa kuwasilishwa katika bunge la Senet ambayo sheria hiyo itawaruhusu watoto kuanzia miaka 10 kupewa mipira ya kondomu na dawa za kupanga uzazi.
Sheria ya afya ya uzazi 2014 ambayo tayari ipo mbele ya Senet,inasema kuwa elimu kwa watoto kuhusu afya ya uzazi na ngono wapewe watoto pengine hata bila ya wazazi kutoa idhini.
Sheria hiyo imewasilishwa na Seneta mteule Bi.Judith Sijeny anayesema kwenye pendekezo la mswada huo kua watoto wanaovunja ungo wapawe nafasi yakutosha kupata habari kamilifu kuhusu elimu ya ngono na huduma za kisiri.
Ikiwa ni pamoja na habari za kutosha na orodha ya dawa za kupanga uzazi na habari kuhusu ujauzito na uzazi wa mpango,muwada huo unaashiria kwamba wanaovunja ungo ni walio kati ya umri wa miaka 10 na 17 ambao ni wanafunzi kati ya darasa la tano na kidato cha tatu.